Rais William Ruto ameelekeza darubini yake katika eneo la Nyanza, akitafuta uungwaji mkono katika azma yake ya kutetea kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, akisema kuwa maslahi ya wakazi wa eneo hilo yatashughulikiwa wakati wa utawala wake. Akihutubia wakazi wa mji wa Kisumu kwenye mzunguko mashuhuri wa Kondele, kiongozi wa taifa alisema mazungumzo yanayoendelea ya kuunda muungano wa kisiasa kati ya vyama vya UDA na ODM, yatalihakikishia eneo hilo nafasi ndani ya serikali na kutimiza ndoto ya aliyekuwa waziri mkuu marehemu Raila Odinga kwa taifa hili kuungana. Na kama mwanahabri wetu Wycliffe Oketch anavyotuharifu, rais pia aliusuta upande wa upinzani akisema wamekosa mwelekeo wa kisiasa.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive