- 314 viewsDuration: 3:53Muungano wa upinzani unataka kukomeshwa kwa mashambulizi na unyanyasaji unaodaiwa kuendelezwa dhidi ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na washirika wake wa kisiasa. Wakizungumza baada ya kukutana na inspekta jeneali wa polisi katika jumba la Vigilance jijini Nairobi, viongozi wa upinzani wakiongozwa na Kalonzo Musyoka na Martha Karua walilaumu huduma ya kitaifa ya polisi kwa kile walichotaja kuwa kukosa kulinda usalama wa viongozi wa upinzani na kukiuka uhuru wao wa kikatiba. Kundi hilo limeonya kuwa litaandaa maandamano iwapo hatua hazitachukuliwa kushughulikia suala hilo. John Kahiro na taarifa kamili. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive