Skip to main content
Skip to main content

Hali ya Hofu Tanzania: Africa Eye inachunguza wimbi la watu kutoweka

  • | BBC Swahili
    18,171 views
    Duration: 51:04
    #BBCAfricaEye inachunguza wimbi la watu kutoweka linaloeneza hofu kote Tanzania. Samia Suluhu alipokuwa rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania mwaka 2021, baada ya kifo cha ghafla cha mtangulizi wake akiwa madarakani, kulikuwa na matumaini kwamba urais wake ungesaidia kuvunja kwa utawala wa kiimla. Aliondoa marufuku ya mikutano ya vyama vya upinzani, akaruhusu vyombo vya habari kufanya kazi kwa uhuru zaidi, na akatoa wito wa ushirikiano na ujumuishaji mpana wa kisiasa. Hata hivyo, matumaini ya mabadiliko ya kudumu yalififia haraka. Kuanzia viongozi wa upinzani na watetezi wa haki za binadamu, hadi wasanii na hata wanachama wa chama tawala chenyewe, msako mkali usio na kifani dhidi ya wakosoaji wa serikali umeitikisa Tanzania. Kupitia ushuhuda mzito wa manusura wa utekaji nyara na mateso, Wakisimulia tena kwa undani mambo ya kutisha waliyopitia filamu hii inafichua kampeni ya vitisho na hofu ambayo wakosoaji wa serikali wanavumilia nchini. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw