Huku zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya makataa ya siku sitini kwa jamii zinazoishi katika kaunti ya Tana River kusalimisha silaha haramu, viongozi kutoka kaunti hiyo wanasema hawajaridhika na idadi ya silaha ambazo zimerejeshwa kufikia sasa.
Wakizungumza mjini Madogo, viongozi hao wamesema baadhi ya wazee wa jamii zingine hawakuitikia wito wa serikali na kushawishi jamii zao kusalimisha silaha hizo na kusababisha zoezi hilo kukosa kufikia matarajio yake. Wamesema utovu wa usalama eneo hilo limehujumu juhudi za maendeleo na kufanya kubaki nyumba kwa miaka mingi.