- 4,021 viewsDuration: 1:39Huku vyama vya kisiasa katika eneo la Magharibi vikizidi kujipanga kuelekea uchaguzi mkuu ujao, wabunge wa chama cha DAP-K kutoka eneo hilo wamejitokeza kwa kauli moja kusisitiza kuwa lazima chama chao kiwe na mgombea wa urais kwenye debe. Wabunge hao wanasema hatua hiyo ni muhimu ili kuhakikisha sauti na maslahi ya eneo la Magharibi yanawakilishwa ipasavyo katika uongozi wa juu wa nchi.