Skip to main content
Skip to main content

Green Army wakusanya taka Nairobi kwa ajili ya kuzalisha umeme

  • | Citizen TV
    355 views
    Duration: 1:55
    Kaunti ya Nairobi Jumapili usiku iliendesha zoezi kubwa la usafi lililoratibiwa kwa lengo la kuimarisha ukusanyaji na utupaji wa taka jijini. Waziri wa Mazingira, Maureen Njeri, amedokeza kuwa zoezi hilo linafanyika sambamba na usafi wa kila siku unaotekelezwa na kikosi cha zaidi ya vijana 4,000 wa “Green Army,” na linaashiria mwanzo wa mpango mpana wa kuboresha mfumo wa usimamizi wa taka. Huku akielezea kuwa kwa ushirikiano na Serikali ya Kitaifa, kaunti inapanga kutumia upya zaidi ya tani tatu za taka zinazokusanywa kila siku kutengeza mbolea na umeme. Zoezi hilo linafuatia tangazo la Rais William Ruto na Gavana Johnson Sakaja kwamba zabuni ya mfumo jumuishi wa usimamizi wa taka jijini imekamilika, huku utekelezaji ukitarajiwa kuanza Aprili Mosi.