Skip to main content
Skip to main content

Shilingi milioni 450 zimetengwa kusomesha wanafunzi Mandera

  • | Citizen TV
    445 views
    Duration: 1:45
    Serikali ya kaunti ya Mandera imezindua mpango wa elimu kwa wote wa kuwalipia karo wanafunzi wa kaunti hiyo, mpango ambao inanuia kuimarisha viwango vya elimu katika eneo hilo. Kwenye mpango huo, wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu watanufaika pakubwa baada ya serikali hiyo kutoa takriban shilingi milioni mia nne na hamsini kwenye kitita hicho. Gavana wa kaunti hiyo Mohammed Khalif amesema mpango huo utasaidia wanafunzi kutoka familia nyingi ambao wamepoteza mifugo yao wakati huu wa ukame.