Ndoa za utotoni zikizidi kuzima ndoto za wasichana wafugaji katika eneo la Loiyangalani kaunti ya Marsabit, mama mmoja ameanza kampeni kuzuia kuongezeka kwa visa hivi. Nakidor Moru, ambaye mwenyewe ni muathiriwa wa ndoa za utotoni na ambaye kwa sasa ni balozi wa kujitolea amekata kauli kuendeleza hamasisho ya kukomesha mila hiyo katika jamii yake. Hata hivyo Nakidor,amekiri mchakato huo unayumbishwa na pingamizi za jamii yake inayomuona kama msaliti. Bonface Barasa, anatuarifu zaidi kuhusu juhudi za Nakidor huko Loiyangalani.