- 48 viewsDuration: 1:59Viongozi wa pwani wamesema wanaunga mkono mpango wa serikali wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa ujenzi wa barabara na nyumba za bei nafuu Wakizungumza eneo la Bughuta kaunti ya Taita Taveta, Waziri wa michezo Salim Mvurya anasema serikali itahakikisha miradi mikuu eneo hilo inakamilika kwa wakati. Mvurya akiahidi kwamba mwanakandarasi wa kutengeneza barabara ya Maungu hadi Kasighau na ile ya Voi kuenda Saghalla amepatikana na kwamba ujenzi wa barabara hizo utaanza hivi karibuni.