- 521 viewsDuration: 1:38Baadhi ya mawakili wamefanya maandamano kulalamikia dhulma za kingono. Mawakili hao, ambao ni wachanga kwenye taaluma hiyo, pamoja na wanagenzi, wanalalamikia kudhulumiwa na baadhi ya mawakili waandamizi. wanasema kuwa hawawezi kukaa kimya ilhali wanapata ugumu wa kufanya kazi zao. aidha wanakitaka chama cha wanasheria nchini kuwalinda kutokana na unyanyasaji wa kingono wakidai kuwa licha ya kuwasilisha malalamishi, LSK imewapuuza waathiriwa.