- 10,383 viewsDuration: 2:52Kauli ya kinara wa ODM Dkt. Oburu Oginga kuwa chungwa linalenga kiti cha naibu rais kwenye uchaguzi MKUU MWAKA ujao, imewagusa pabaya viongozi wa UDA, haswa kutoka maeneo ya Mlima Kenya. Viongozi hao wamesema kamwe hawatakubali kumsulubisha Profesa Kithure Kindiki kwa kutafuta uungwaji mkono na ODM. Na kama anavyoarifu Melita Oletenges, Viongozi hao wanasisitiza kuwa wana imani na Kindiki kuendelea kuhifadhi kiti hicho kwenye kinyang'anyiro kijacho.