- 260 viewsDuration: 3:13Ukosefu wa mtandao wa simu umewaathiri wakazi wa kijiji cha Nkutuk Eng'iron Samburu mashariki, ambao wanakosa mbinu ya kuwasiliana na wenzao, mbali na hali hiyo kuathiri usalama katika eneo hilo. Wakazi wanasema majangili hutumia fursa hiyo kuendelea na mashambulizi ya wizi wa mifugo wakifahamu ni vigumu kwa wenyeji kutafuta usaidizi kutoka kwa maafisa wa polisi.