Waziri wa usalama Kithure Kindiki aonya magenge ya wahalifu Nairobi

  • | Citizen TV
    1,073 views

    Waziri wa usalama wa kitaifa, Kithure Kindiki, ametoa onyo kali kwa magenge ya wahalifu yanayohangaisha wakaazi wa Nairobi. Kindiki leo amefanya ziara ya kutathmini hali ya usalama katikati mwa jiji la Nairobi na haswa soko la Muthurwa, ambapo amefanya mashauriano mafupi na wakaazi na wafanyibiashara. Waziri kindiki akionekana kuzungumza na watu wa sekta mbalimbali kutathmini hali, huku akiahidi kuwa wizara yake itasimama imara kuhakikisha hali salama jijini. Waziri akiahidi kuongezwa kwa doria za maafisa wa usalama katika maeneo yenye visa zaidi vya uhalifu.