Skip to main content
Skip to main content

Mkewe mkuu wa mawaziri ataka vikwazo vya kisheria vinavyozuia usawa wa kijinsia viondolewe

  • | Citizen TV
    163 views
    Duration: 1:35
    Mkewe mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi, Tessie Mudavadi, alitoa wito wa kuondoa vizuizi vya kisheria na miundo vinavyozuia kupatikana kwa usawa wa kijinsia. Akizungumza wakati wa sherehe za Siku ya Wanawake Duniani katika Kaunti ya Tharaka Nithi, Tessie alisisitiza kuwa kuondoa vizuizi vya haki kwa wanawake na wasichana ni muhimu kwa maendeleo ya kitaifa. aliyasema hayo wakati wa kutoa msaada wa vivungulio vya watoto vilivyotolewa na wakfu wa Ushirika Wema kwenye mpango wa Okoa Malaika katika hospitali ya chuka level five.