Waziri wa usalama asema polisi wataongezewa silaha

  • | Citizen TV
    910 views

    Waziri wa usalama wa kitaifa Profesa Kithure Kindiki ametangaza kuwa serikali imeweka mikakati ya kuongeza vifaa vya usalama kwa maafisa wanaolinda maeneo yaliyoathirika na ukosefu wa usalama kutokana na wizi wa mifugo. Waziri Kindiki aliyezungumza alipozuru eneo la Kakuma na maeneo mengine kaunti ya Turkana, pia amewaonya wafadhili wa wezi wa mifugo na wahalifu ambao wamewahangaisha wakaazi wa Turkana na sehemu za bonde la ufa kuwa serikali itakabiliana nao kikamilifu.