Utoaji mikopo kwa makundi wasaidia kuhifadhi mazingira

  • | K24 Video
    53 views

    Jamii zinazoishi katika Pwani ya kenya huathirika kwa njia moja au nyingine, kutokana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo hupelekea maji ya bahari kuvunja kingo na kuharibu mashamba na mali zao. Ili kupiga jeki uhifadhi wa mikoko na mazingira kwa jumla, shirika moja lisilokuwa la serikali kwa jina comred, linatoa mikopo kwa makundi ya uhifadhi yaliyosajiliwa, ili kuwapa motisha wanachama. Kufikia sasa makundi mbali mbali yamepokea mikopo, ambayo inajulikana kama Eco-credit ambayo huitumia kujiinua kimaisha huku mazingira yakitunzwa.