Naibu Rais William Ruto aadhinishwa na IEBC kugombea urais

  • | K24 Video
    173 views

    Naibu Rais William Ruto ameidhinishwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka , IEBC kugombea urais katika uchaguzi wa Agosti tisa. Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amemkabidhi Ruto cheti cha ugombeaji baada ya kuafikia masharti yote ya kugombea urais. Ruto alitumia fursa hiyo kuitaka IEBC ifanye kazi kwa mujibu wa katiba huku akivitaka vyombo vya habari visiwe na ubaguzi.