Idara ya Mahakama yalalamikia ukosefu wa pesa kuendeleza miradi ya miundo msingi

  • | Citizen TV
    306 views

    Idara ya Mahakama inalalamikia ukosefu wa pesa kama sababu ya wao kukosa uwezo wa kuendeleza miradi ya miundombinu haswa ujenzi wa majengo ya Mahakama. Akizungumza katika Kaunti ya Siaya wakati wa uzinduzi rasmi wa jengo la Mahakama Kuu ya Siaya, Jaji William Ouko, ambaye anaongoza kamati ya miundomsingi katika idara ya mahakama amelalamikia mgao mdogo ambao wamekuwa wakipokea kutoka kwa hazina ya taifa ambayo wanasema haiwezi hata kukamilisha mradi mmoja wa ujenzi wa mahakama ya kisasa.