- 8,050 viewsDuration: 1:22Mshtuko na huzuni zimegubika kijiji cha Kanorero eneo la Kangema, kaunti ya Murang'a baada ya mama mmoja kuwadunga kisu wanawe watatuwenye umri wa miaka 7, minne na miwili. Wawili kati yao walifariki papo hapo huku mmoja sasa akisalia kupigania uhai katika hospitali ya Murang'a level 5. Mwanamke huyo baadaye alijaribu kujidunga kisu kabla ya kujiwasilisha katika kituo cha polisi cha Kanorero. Inadaiwa kuwa mama huyo aliwauwa wanawe kufuatia ugomvi na mumewe. Maiti ya watoto hao ilipelekwa katika makafani ya Kangema.