- 1,041 viewsDuration: 2:34Serikali sasa imesitisha mpango wa msaada wa chakula kwa wanafunzi unaoendelezwa na Shirika moja la kihindu. Hii ni kufuatia taarifa kuwa wanafunzi wanaopokea msaada huo wa chakula katika shule 17 eneo la Ganze kaunti ya Kilifi wamekuwa wakilazimishwa kufanya maombi ya kihindu kabla ya kupokea msaada. Na kama anavyoarifu Chrispine Otieno Kamishna wa Kilifi JOSPHAT BIWOTT amesema kuwa uchunguzi umeanzishwa kufuatia kuibuka kwa kanda ya video inayowaonyesha wanafunzi hao wakisali kihindu.