- 19 viewsWakazi wa Kajiado walijumuika kwenye matembezi ya zaidi ya kilomita 12 , huku wakivuta kitambaa cheupe cha urefu wa kilomita 12 kama ishara ya mshikamano na kudumisha amani. Matembezi haya yalilenga kuonyesha umuhimu wa kuzima vita kote duniani na kuhimiza mshikamano wa kijamii. Washiriki, wakiwemo wakristo na waislamu, walipigia debe amani nchini na kutoa wito kwa kaunti zingine kuiga mfano huo.