Skip to main content
Skip to main content

Maadhimisho ya usafi wa mazingira duniani yafanyika Machakos

  • | Citizen TV
    197 views
    Duration: 1:27
    Mji wa Machakos ulikuwa mwenyeji wa maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Usafi Duniani, ambapo wito ulitolewa kwa Wakenya kuzingatia kukusanya taka hasa za nguo. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira – NEMA, yaliwaleta pamoja wadau mbalimbali, vikundi vya vijana, na wakazi kwa matembezi ya uhamasishaji na ukusanyaji wa takataka. Maadhimisho ya mwaka huu yaliandaliwa chini ya kauli mbiu: “Kufuatilia Taka za Nguo na Mitindo Kupitia Mitindo Endelevu,” yakilenga changamoto inayoibuka ya uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na taka za nguo.