- 6,362 viewsDuration: 1:10Ujenzi wa barabara ya Mombasa kuelekea kilifi unatazamiwa kuendelea baada ya serikali kuanza kulipa fidia kwa watakaothirika na ukarabati wa barabara hiyo. Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya barabara kuu nchini Luka kimeli amedokeza kuwa mkandarasi atahitajika kufanya kazi saa 24 ili kuhakikisha ujenzi wa barabara kutoka lights hadi bombululu umekamilika haraka. Aidha sehemu ya kutoka Bamburi junction hadi mtwapa inatazamiwa kufunguliwa kwa uchukuzi mwezi oktoba .