- 80 viewsWananchi wa Haiti katika mji mkuu wa Port-au-Prince na vitongoji jirani wako mbiyoni wiki nzima hivi sasa bila ya kujuwa wapi watakwenda kutokana na mapigano kati ya magenge ya uhalifu na polisi. Ghasia hiso zilizuka wiki moja iliyopita na kuilazimisha serikali kutangaza hali ya dharura, na Marekani kuwaondoa raia wake kuanzia Jumapili. Hali katika nchi hiyo ya Caribean inaripotiwa kuwa mbaya sana na kuisababisha Jumuiya ya kimataifa kueleza wasi wasi wake na kutoa wito wa kusitisha ghasia na kudumisha amani. Wakazi wa mji mkuu wa Port-au-Prince wanazidi kukabiliwa na hali mbaya ya maisha bila ya chakula, maji wala mahali yakuishi kutokana na mapigano ya magengi yanayoendelea kwa zaidi ya wiki moja sasa kati ya magengi ya wahuni na polisi. Filienne Setoute ameliambia Shirika la Habari la AFP kwamba amefanya kazi kwa miaka 20 katika wizara ya huduma za jamii na ajira, na kuweza kujijengea nyumba yake, lakini hivi sasa hana tena mahali ya kulala. Filienne Setoute mfanyakazi wa wizara ya huduma za jamii: “Hatujaweza kulala kwa siku mbili hivi sasa. Tunakimbia, mimi na vitu vyangu kichwani bila ya kujuwa ninakwenda wapi. Nilikua na nyumba yangu lakini sasa sina makazi tena. Kilio hicho kinaelezwa na mamia ya Wahaiti waliokuwa wanakimbia wakilaumu polisi kushindwa kufanya kazi zao.” Reginald Bistol raia aliyepoteza makazi yake anasema: “Hapa ni suala la kufa au kupona, hatuna la kufanya, hakuna tofauti kati ya nyumba za watu binafsi na mali ya umaa. Hebu fikiria, tukiuliwa sote hapa Port-au-Prince, haya majengo yatakua na maana gani? Wahuni wametulazimisha kuondoka kutoka makazi yetu, tumepoteza kila kitu tulokua nacho, tumepoteza familia. Sasa tuko barabarani.” Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limesema mwishoni mwa wiki kwamba karibu Wahaiti laki tatu elfu sitini na mbili wamekoseshwa makazi tangu kuzuka kwa ghasia hizi. - VOA, AFP, AP, Reuters #haiti #magenge #polisi #wananchi #mauaji #wakimbizi #voa #voaswahili #carribean
Mapigano kati ya magenge ya uhalifu na polisi yaendelea
- 12 Aug 2025 - Douglas Kamau says he narrowly escaped death when a bullet struck his arm and ribs, allegedly fired by a police officer from Makutano Police Station.
- 12 Aug 2025 - Naivasha Senior Resident Magistrate Wilson Rading on Monday recused himself from hearing the case against 73-year-old farmer Francis Muya, who is accused of plotting to kill five members of his family.
- 12 Aug 2025 - While Chirchir is of the opinion that road crashes are “preventable if all road users play their part” the Motorists Association of Kenya (MAK) has placed blame on government agencies.
- 12 Aug 2025 - The Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) has 9 governors on its radar over corruption cases as it intensifies its crackdown on nationwide graft.
- 12 Aug 2025 - Prosecutors in the Ivory Coast said Monday they have charged 11 people, including members of the opposition party of ex-president Laurent Gbagbo, with alleged "terrorist" offences linked to unrest earlier this month.
- 12 Aug 2025 - Authorities in Taiwan were scrambling on Tuesday to evacuate hundreds ahead of a possible landfall by Typhoon Podul on the island's southeastern coast, while nearby areas battle to recover from floods and record winds brought by previous storms.
- 12 Aug 2025 - Hundreds of cabin crew members took their fight to major Canadian airports on Monday, picketing against unpaid labor, as talks on wages intensify between Air Canada AC.TO and its flight attendants this week ahead of a possible strike.
- 12 Aug 2025 - Condemnations poured in from the United Nations, the EU and media rights groups Monday after an Israeli strike killed an Al Jazeera news team in Gaza, as Palestinians mourned the journalists and Israel accused one of them of being a Hamas militant.
- 12 Aug 2025 - Scientists have discovered the fossil of a tiny mouse-sized mammal that lived in the time of the dinosaurs in Chilean Patagonia.
- 12 Aug 2025 - Govt has announced privatisation plans for some of the biggest State companies.