Skip to main content
Skip to main content

Usajili wa makurutu wa polisi

  • | Citizen TV
    1,726 views
    Duration: 2:00
    Idara ya Huduma ya Polisi inatarajia kuanza zoezi la kuajiri maafisa wa polisi Ijumaa tarehe 3O Oktoba, ikilenga askari wapya 10,000 kote nchini. Kulingana na Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja, uzinduzi huo pia utaashiria mwanzo wa mchakato wa uajiri wa siku tano ambao kwa mara ya kwanza utaendeshwa kwa pamoja na Tume ya Huduma za Polisi (NPSC). Amani Kamora, Mwenyekiti wa NPSC, amesisitiza haja ya uwazi na haki, akionya kuwa aina yoyote ya ufisadi iwe kutoa au kupokea hongo itakabiliwa nakisheria. IPOA na mashirika mengine ya usimamizi yatakuwepo kufuatilia mchakato huo.