- 2,179 viewsDuration: 2:15Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amesema kwamba oparesheni maalum ya kukamata magenge ya uhalifu katikati mwa jiji la Nairobi na mitaani tayari imeanzishwa na vitengo mbali mbali vya usalama. Akizungumza kwenye Jukwaa la Usalama katika kaunti ya Nairobi, waziri Murkomen amesema kwamba serikali itazindua miradi mbali mbali ya kuwapa vijana ajira na kupiga jeki sekta ya michezo ili kupiga jeki ukuzaji wa Talanta. Kikao hicho kinaendelea katika Chuo kikuu cha Serikali, huko Kabete.