Usajili wa wapiga kura ukishuhudia idadi ndogo ya wanaojitokeza kusajiliwa katika maeneo mengi nchini, juhudi za kuwarai wakenya na haswa vijana kujisajili zimeanza mashinani. Huko Nyeri, ambako ni wapiga kura 30 tu waliosajiliwa tangu zoezi hilo kuanza, kundi la vijana wameungana na kuanza kuwafikia wenzao mitaani na vijijini kuwarai kujisajili ili kuleta mabadiliko kwenye uchaguzi mkuu ujao. Na kama anavyoarifu sasa Kamau Mwangi, Juhudi hizo zimeanza huku IEBC ikitangaza kuwa wapiga kura wapya elfu saba arobaini na wanane walisajiliwa wiki ya kwanzaya shughuli hiyo.