- 1,423 viewsDuration: 2:58Familia moja eneo la Kisaju kaunti ya Kajiado inahangaika baada ya mtoto wao wa miaka miwili kupotea kutoka kituo cha kutwa cha kulea watoto. Mamake mtoto aliyetoweka anasema kuwa msimamisi wa kituo hicho aliondoka kumpelekea mwanawe chakula shuleni na kuwaacha watoto watano kituoni, lakini mtoto huyo hakuwepo aliporejea. Familia ya mtoto huyo imekuwa ikimtafuta kwa siku 25 sasa bila mafanikio yoyote.