Chama cha KANU kimeshindwa kwenye kesi iliyotaka kurejeshewa umiliki wa jumba la KICC

  • | KBC Video
    75 views

    Chama cha KANU kimeshindwa kwenye kesi iliyowasilishwa kutaka kurejeshewa umiliki wa jumba la mikutano ya kimataifa la KICC. Mahakama ya kushughulikia mizozo kuhusu mazingira na ardhi imetoa uamuzi kuwa ardhi ambayo jumba hilo limejengwa inamilikiwa na serikali baada ya kubatilisha hatimiliki iliyotolewa kwa chama hicho. Akitoa uamuzi kuhusu suala hilo, Jaji Jacqueline Mogeni alisema ugawaji wa ardhi kwa KANU bila kufuata utaratibu ni kinyume cha sheria na katiba. Ruth Wamboi anaarifu zaidi kwenye mizani ya haki.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive