Kiwanda cha nguo chazinduliwa katika kaunti ya Mombasa

  • | Citizen TV
    822 views

    Balozi wa Marekani nchini Meg Whitman ameitaka serikali kuu na zile za kaunti kuwekeza katika miradi inayolenga kutoa ajira kwa vijana. Akizungumza huko mombasa katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha nguo amesema ukosefu wa kazi ukechangia katika ongezeko la uhalifu,kudorora kwa usalama na uchumi kufifia pia. Gavana wa Mombasa aliyehudhuria hafla hiyo amesema kuwepo kwa bandari kunatoa fursa kwa wawekezaji kujenga kampuni ili kurahisisha usafirishaji wa shehena zao.