Sherehe ya kumtuza David Koi yaandaliwa Kilifi

  • | Citizen TV
    507 views

    Makavazi ya Kitaifa kwa ushirikiano na kanisa la ACK yaliandaa sherehe maalum ya kumtuza David koi ambaye alikuwa mmoja wa walioweka juhudi za kukomesha biashara ya utumwa katika ukanda wa pwani na Afrika mashariki. katika hafla iliyoandaliwa katika eneo la Gede kaunti ya kilifi, wakaazi na Viongozi wa kaunti hiyo walipata nafasi ya kumfahamu shujaa huyo. Maafisa wa makavazi ya kitaifa wamesema kuwa kuna haja ya ushirikiano zaidi kati ya serikali ya kaunti na wafadhili ili kujenga mnara wa ukumbusho wa shujaa huyo.