Wavuvi na wafanyibiashara wataka vifaa vya kusafisha fuo za bahari huko Kwale

  • | Citizen TV
    394 views

    Wavuvi na wafanyibiashara wa baharini katika eneo la Msambweni kaunti ya Kwale wametaka serikali kuu na ya kaunti kutoa vifaa vya kusafisha bahari na kutunza mikoko ili kulinda mazingira ya baharini. Wakizungumza katika zoezi la kuzoa taka baharini eneo la Mwakamba na upanzi wa mikoko huko Makongeni wadau hao wamesema juhudi zao za kutunza mazingira ya bahari zimesababisha fuo za Diani kutambulika ulimwenguni na kutuzwa kama ufuo bora zaidi barani Afrika kwa mara ya nane.