
223,390 views
7 Feb 2025
STANZA 1 Siku iliwekwa Wayahudi walipaswa kuharibiwa na mali zao kuchukuliwa.Amri ya Wamedi na Waajemi haikuweza kubatilishwa. Shetani alitaka kuwaondoa duniani waliohifadhi ujuzi wa Mungu wa kweli Lakini Esta malkia alijitosa mbele ya mfalme Ahusuero kama mwombezi, naye Bwana alitimiza ukombozi mkuu kwa watu wake CHORUS Nani ajuaye kwamba umeujia ufalme kwa wakati kama huu? swali liliulizwa malkia Esta katika msiba huu. Wayahudi Shushan waliomba na kufunga kukawa na wokovu kwao. Nasi leo tunapopambana na maadui wa kweli ndugu , twapaswa kudumisha uaminifu wetu kwa Mungu kama Esta, twapaswa kudumisha uaminifu Kristo aje kutukomboa. STANZA 2 Leo huyu Joka afanya vita juu ya wazao wasalia, wazishikao amri za Mungu. Amri itatolewa dhidi yenu kama ile dhidi ya Wayahudi. Kwa uwakilishi wao wa uongo na rufaa za hasira, watachochea tamaa za watu lakini wanaomcha Mungu wao, hawawezi kukubali taasisi hiyo, inayokiuka kanuni za maagizo walopewa naye Mungu Mkuu, watakombolewa.