Skip to main content
Skip to main content

Abdihamid Hassan ashinda shindano la uvumbuzi kwa kuvumbua mfumo wa akiliunde wa kudhibiti ukame

  • | Citizen TV
    330 views
    Duration: 1:56
    Abdihamid Hassan kutoka kaunti ya Isiolo ndiye mshindi wa mashindano ya kitaifa ya ubunifu wa teknolojia. Mfumo wake aliobuni unatumia akiliunde kukusanya data za setilaiti kuhusu ukame na lishe kwa mifugo na kisha kuwaarifu wafugaji moja kwa moja kwa kuwapigia simu. Mfumo huo uliteuliwa kama ubunifu bora zaidi katika mashindano ya Red Bull Basement yaliofanyika katika kituo cha Ihub hapa jijini Nairobi. Abdihamid sasa atawakilisha Kenya katika mashindano ya kimataifa huko Silicon Valley, Marekani, mwezi wa sita kwa huu.