- 521 viewsDuration: 1:52Kikundi cha wakazi wa Kaunti ya Kericho kimeenda mahakamani kikiomba maagizo ya kurejeshwa kwa vipande viwili vya ardhi ambavyo kwa sasa vinadhibitiwa na Kampuni ya Sukari ya Muhoroni. Katika ombi walilowasilisha katika Mahakama ya Mazingira na Ardhi Kericho, wakazi hao wanaomba mahakama itangaze kuwa Serikali ya Kaunti ya Kericho ndiyo mmiliki halali wa mashamba hayo kwa niaba ya jamii ya eneo hilo.