Skip to main content
Skip to main content

Baraza la magavana wafika mbele ya kamati ya seneti ya fedha na bajeti na kupendekeza mgao wa shilin

  • | Citizen TV
    216 views
    Duration: 2:04
    Baraza la magavana limetaka mgao wa shilingi bilioni 534 katika mwaka ujao wa kifedha. Mwenyekiti wa COG Ahmed Abdulahi akisema kaunti zinahitaji fedha zaidi ya kuwalipa wafanyakazi na majukumu mengine ya kaunti. Akizungumza mbele ya kamati ya seneti hii leo mwenyekiti wa tume ya ugavi wa rasilmali nchini CRA, Mary Chebukati alipendekeza kaunti kupewa shilingi bilioni 458.9 katika mwaka wa kifedha wa 2026/2027, akisema matumizi ya kaunti yameongezeka. Katika mwaka huu wa kifedha, kaunti zimepokea shilingi bilioni 415.