- 552 viewsDuration: 2:04Baadhi ya wazee na wakazi wa Kaunti ya Isiolo wameitaka serikali ya kitaifa kuchukua hatua za haraka kutatua mgogoro wa uongozi unaoendelea kushuhudiwa katika Kaunti hiyo. Aidha wazee hao wamesema kuwa mvutano huo umezaa mabunge mawili pinzani, bajeti tata, hali ya ukosefu wa usalama na madai ya ufisadi ambayo yamelemaza utoaji wa huduma na kuiweka Kaunti hio katika hatari ya kusambaratika kabisa.