- 17,458 viewsDuration: 1:59BBC imepata video za raia wa Urusi anayedai kufanya hujuma nchini humo kwa niaba ya Ukraine kwa kipindi cha miaka miwili. Mwanamume huyo, anayetumia jina la Ivan ambalo si jina lake halisi, alituma video hizo kwa mwandishi wa habari wa Poland. Anadai kuwa amesaidia kutekeleza mashambulizi dhidi ya maeneo ya kijeshi ya Urusi kwa niaba ya Ukraine, lakini anasema hajawahi kulenga raia. Katika uchunguzi wa BBC imethibitisha kuwa Ivan anafanya kazi kwa idara ya ujasusi ya Ukraine, lakini haijaweza kujithibitishia kwa uhuru operesheni anazodai kushiriki. #bbcswahili #bbceye #urusi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw