Skip to main content
Skip to main content

BBC News Swahili

  • | BBC Swahili
    54,498 views
    Duration: 1:11
    Rais wa Marekani, Donald Trump, amezua mjadala mitandaoni baada ya kumsifu msanii wa muziki wa rap, Nicki Minaj, kuhusu muonekano wake wakati wa mkutano wa kisiasa wa chama cha Republican uliofanyika Michigan. Trump alitoa kauli hiyo Jumapili, Oktoba 25, baada ya Minaj kusafiri naye kwa ndege ya rais, Air Force One, kuelekea mkutanoni. Kauli hiyo imevuta hisia za watumiaji wa mitandao ya kijamii, na kuzua mjadala kuhusu namna rais huyo anavyozungumzia mwonekano wa wanawake hadharani. Mwandishi wa BBC @sarafinarobi na taarifa hii - - #bbcswahili #marekani #trump #nickminaj #foryou Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw