Skip to main content
Skip to main content

Bwawa la umeme Tanzania litashusha bei ya umeme?

  • | BBC Swahili
    35,497 views
    Duration: 1:28
    Je, kukamilika kwa Mradi wa uzalishaji umeme wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) kutawawezesha wananchi kulipia umeme kwa bei nafuu? Mradi wa uzalishaji umeme wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) umezinduliwa rasmi nchini Tanzania, huku ukitarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji wa umeme nchini. Kupitia mahojiano maalumu na mwandishi wa BBC Yusuph Mazimu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchemsi Mramba, amesema kuwa licha ya bei ya umeme kutopanda kwa zaidi ya miaka 10, kuna vigezo mbalimbali vinavyozingatiwa na mamlaka husika katika kupanga bei ya umeme kabla ya kufanya uamuzi wa kuishusha au kuipandisha. 🎥: @frankmavura #bbcswahili #jnhpp #nishati Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw