- 24,200 viewsDuration: 46sChama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kimesema kimewasilisha barua rasmi kwa Rais wa Kenya, William Ruto ya kumuomba kuingilia kati suala la madai ya kutekwa kwa Mwanaharakati Twaha Mwaipaya. Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Oktoba 27, 2026 Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema barua hiyo imewasilishwa leo katika Ofisi za Ubalozi wa Kenya Nchini Tanzania, ikiwa na kichwa cha habari kinachosomeka "Urgently Appeal for Your Personal Intervention in the Abduction of Twaha Mwaipaya and Protection of Democratic Activists in East Africa." Kupitia barua hiyo, CHADEMA imemuomba Rais Ruto kutumia nafasi yake kuingilia kati suala hilo, huku kikisisitiza umuhimu wa kulinda usalama wa Wanaharakati wa Demokrasia katika Ukanda wa Afrika Masharikl. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw