- 1,505 viewsDuration: 3:48Idadi ndogo ya wapiga kura imeshuhudiwa katika vituo mbalimbali vya kupigia kura katika wadi za Nyamaiya, Ekerenyo na Nyansiongo katika kaunti ya Nyamira. Kura zikionekana kupigwa kwa amani katika maeneo mengi japo kisa kimoja cha vurugu kulishuhudiwa katika wadi ya Nyamaiya, ambapo magari mawili ya wawaniaji wawili yalivamiwa na kupigwa mawe na watu wasiojulikana.