- 327 viewsDuration: 2:21Muungano wa walimu wa shule za upili na vyuo vya mnafunzo anuai nchini KUPPET sasa unalitaka bunge la kitaifa kupitisha sheria ya kuwapa walimu wa shule za sekondari msingi uwezo wa kujisimamia kando na serikali kuimarisha bima ya SHA la sivyo watagoma. Wakiongozwa na makatibu wa KUPPET kutoka matawi mbali mbali humu nchini wamesema kuwa walimu hasa wale wanaougua saratani wanakosa huduma kupitia bima ya SHA licha ya kuwepo kwa mkataba unaojumuisha matibabu ya ugonjwa huo. walikuwa wakikizungumza na wanahabari mjini Malindi katika mashindano ya walimu wa shule za sekondari na sekondari msingi .