- 236 viewsDuration: 2:01Chama cha National Economic Development Party ( NEDP) kimesema wahudumu wa afya wa vitengo mbalimbali wanapaswa kukumbukwa na kutuzwa mara kwa mara kwa kuwa huwa wanasahaulika licha ya kuwa mstari wa mbele kuokoa maisha ya wagonjwa hospitalini. Akizungumza wakati wa zoezi la kutoa damu na kuwazawadi wahudumu hao katika hospitali ya Msambweni kaunti ya Kwale, mwakilishi wa chama hicho Samuel Kimathi amesema wahudumu wengi wa afya hupitia hali ngumu za kikazi na hata kupatwa na msongo wa mawazo kutokana na hali hizo.