- 1,848 viewsDuration: 2:06Uongozi wa chama cha United Progressive Alliance( UPA) sasa umeamua kwamba katika uchaguzi ujao chama hicho kitakuwa na wagombea katika nyadhifa zote za kisiasa ila tu katika kiti cha mgombea urais . Katika mkutano maalum ya wajumbe wakuu na viongozi wa mashinani wa chama hicho ilioandaliwa kule Kisii, uongozi wa chama hicho umeafikiana kwamba UPA kitaunga mkono mgombea kiti cha Urais Dkt Fred Matiangi ambaye pia ndiye naibu kiongozi wa chama cha Jubilee.