Changamoto zashuhudiwa katika baadhi ya maeneo katika uchaguzi wa UDA

  • | Citizen TV
    857 views

    Uchaguzi wa mashinani wa chama UDA ulianza katika maeneo kadhaa nchini huku shughuli hiyo ikikumbwa na changamoto katika baadhi ya maeneo. Katika kaunti ya Nairobi, Gavana wa Nairobi ni mmoja wa wale waliojipata katika hali hiyo baada ya jina lake kukosekana katika sajili ya chama.Zoezi hilo limeanza kuchelewa katika maeneo kadhaa huku vifaa vya kupigia kura vikiibiwa katika baadhi ya maeneo ya kupigia kura