- 2,091 viewsMaafisa wa upelelezi wanaochunguza mauaji ya Patience Mumbe mwenye umri wa miaka 12 wamepata kanda za CCTV wanazotarajia zitasaidia katika uchunguzi. Mumbe aliyepatikana ameuawa na mwili wake kutupwa Embakasi aliondoka nyumbani alhamisi wiki jana asijulikane alikoenda. Kamera za CCTV zikimnasa akikimbia kuelekea kituo cha magari cha Taj Mall kabla ya kupatikana maiti.