- 87 viewsDuration: 2:01Katika ulimwengu wa kidijitali ambako ushawishi unazidi kuwa sehemu maalum inayoweza kuingiza kipato. fursa mpya imejitokeza kwa kizazi kijacho cha wabunifu nchini Kenya. Shule ya Dentsu school of influence imezindua kundi lake la pili ili kuwapa wabunifu chipukizi ujuzi wa uundaji wa maudhui, kujijenga kama wasanii na njia za kujipatia kipato. Mpango huo pia unaunganisha washiriki na kampuni mbalimbali, ukifungua fursa za ushirikiano, ajira na ukuaji wa kipato katika sekta ya kidijitali.