Waziri wa afya Aden Duale ameelezea wasiwasi na ongezeko la visa vya utumizi mbaya wa bima ya afya ya SHA, akionya kuwa ulaghai wa hospitali za kibinafsi umeathiri huduma katika hospitali za umma haswa eneo la kaskazini mwa Kenya. Akizungumza katika eneo la Habaswein kaunti ya Wajir, Duale amefichua kuwa SHA imelipa bilioni 1.9 katika muda wa mwaka mmoja uliopita, shilingi bilioni 1.5 zikilipwa hospitali za umma. Aidha sasa imebainika kuwa pesa nyingi zimepotea kwa baadhi ya watu kwalipia gharama za matibabu jamaa zao ambao hawajasajiliwa na SHA