Skip to main content
Skip to main content

EPRA yapandisha bei ya petroli kwa Ksh. 28.69 na dizeli kwa Ksh. 40.30 kwa lita

  • | Citizen TV
    484 views
    Duration: 1:05
    Wakenya wameamkia siku nyingine ya bei ghali ya mafuta ya petroli kwa kiwango cha juu zaidi kuwahi kutangazwa, licha ya serikali kusisitiza kuwa taifa lina akiba ya kutosha ya mafuta ya petroli. Mamlaka ya kudhibiti kawi na petroli EPRA imeongeza bei ya mafuta ya petroli kwa shilingi 28.69 kwa lita, huku dizeli ikiongezwa kwa shilingi 40.30 kwa lita. Hapa Nairobi, lita moja ya petroli itauzwa kwa shilingi 206.97 nayo dizeli ikiuzwa kwa shilingi 206.84. hata hivyo bei ya mafuta ya taa haikupandshwa, kwa hivyo itasalia kuwa shilingi 152.78 kwa lita.